CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 16
Lugha ya pamoja iliwasaidia kufanya nini?
From Test 13 — Karatasi ya Marudio 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
Hadithi
Hapo zamani za kale, katika msitu wa furaha, wanyama waliamua kujifunza lugha moja ili waweze kuelewana vizuri. Awali, kila mnyama alikuwa na sauti yake. Simba aliguruma, ndege wakapiga kelele, na fisi wakacheka. Hivyo walishindwa kufanya kazi pamoja.
Siku moja, bundi mwenye hekima aliwaita mkutanoni. Akawaambia, "Tukijifunza lugha moja, tutaishi kwa amani na kusaidiana." Wanyama wote walikubaliana wakaamua kutumia lugha ya pamoja. Ambayo kila mmoja angeweza kuelewa.
Baada ya miezi michache ya mafunzo, wanyama wakaanza kuzungumza kwa lugha moja mambo yakawa mazuri. Walishirikiana kujenga makazi, kutafuta chakula na kuishi kwa amani. Lakini fisi mmoja aliyeitwa choyo alianza kutumia maneno mabaya kwa wenzake. Hapo wanyama waligundua kuwa lugha nzuri huleta umoja lakini maneno mabaya huleta chuki.
Tangu siku hiyo, walikubaliana kuwa watatumia lugha kwa heshima, ili msitu wao uendelee kuwa wa amani.

- AKupigana
- BKusaidiana na kuishi kwa amani
- CKuwinda wenzao
- DKujigamba
Answer
B. Kusaidiana na kuishi kwa amani
Hadithi inasema baada ya kutumia lugha moja "Walishirikiana kujenga makazi, kutafuta chakula na kuishi kwa amani."