naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 2

Sherehe yenyewe ilikuwa siku gani ya juma?

From Kiswahili — End Term 1 Assessment 2025 (Set 4) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 1 hadi la 7.
Mipango yote ya sherehe ya kuzaliwa kwa baba yangu ilikuwa imepangwa ikapangika. Ilikuwa siku ya tatu ya juma. Baba alikuwa akikamilisha miaka thelathini na tisa. Yeye hakuwa amekula chumvi nyingi kama alivyokuwa babaye Meishisana.
Mapochopocho ya vyakula mbalimbali yalikuwa yakinukia mezani na hata mekoni. Vyakula kama vile pilau, biriani, maandazi na vibanzi vilivutia sana machoni pa wageni watano waalikwa. Nilishangaa nilipomwona Bwana Kauleni akidondokwa na mate kwa sababu ya kuitamani keki yenyewe. Watu wengine ambao sikuwatambua kwa majina yao, walikuwa wameketi kitako sebuleni huku wamejipamba kweli kweli. Bila shaka wote walijawa na tabasamu nyusoni pao. Keki yenyewe ilikuwa tamu kama halua. Mimi mwenyewe nilihusika kwa kuwakaribisha marafiki zangu kwenye viti baada ya kuvipanga.

2. Sherehe yenyewe ilikuwa siku gani ya juma?

Answer

Siku ya tatu ya juma.

"Ilikuwa siku ya tatu ya juma."

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test