naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 4

Kutokana na aya ya pili, msichana aliupangiwa kuozwa kwa nani?

From Kiswahili — Monitoring Learner's Progress 2025 (Set 11A) · 2 marks · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Ilikuwa jioni moja wakati walikizo mzee Tamaa alipofika kwetu. Alisindikizwa na wazee wenzake wane. Nilikuwa nimefichwa katika nyumba ya nyanya yangu. Nilikuwa na uoga kama kunguru. Sikujua kwa nini nilifichwa. Wakati huu wote mwili wangu ulitetemeka kama jani la mgomba wakati wa upepo mkali. Nilimuomba Mungu aniokoe kama nilikuwa nimepangiwa kuozwa.
Akilini nilipitiwa na mawazo mengi. Nilikumbuka wasichana walipangiwa kuozwa mapema lakini wakaokolewa na maafisa wa kulinda haki za watoto. Wasichana hao waliokolewa na wakaendelea na masomo yao. Nikiwa nimefichwa nilisikia watu wakizungumza nyumbani kwetu. Nilitegasikio. Nikafahamu kuwa kumbe nilikuwa niozwe kwake mzee Tamaa. Nilizidi kuwaza na kuwazuia na mnaya kujiokoa bila kupata jibu. Sikutaka kukatiza masomo yangu.
Mara mlango ulifunguliwa. Nilishtuka sana. Nikajua wakati niliohofia ulikuwa umefika. Nilipotazama nje, sikuamini macho yangu. Nilimuona chifu amesimama nje ya mlango akiwa na askari. Mzee Tamaa na wenzake walikuwa wamekamatwa. Mipango yao ilikuwa imefika mwisho. Hapo nikawa nimeokolewa kutokana na ndoa ya lazima.

4. Kutokana na aya ya pili, msichana aliupangiwa kuozwa kwa nani?

Answer

Mzee Tamaa

"nilikuwa niozwe kwake mzee Tamaa".

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test