CBC Grade 4 Kiswahili End Term 2 Exam 2026 · Question 4
Mtoto mwenye tabia mbaya ___ na watu wote.
From Kiswahili — Term 2 End-term Assessment 2026 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
Soma hadithi kisha ujibu maswali yafuatayo.
Mwalimu wetu alituambia kwamba ni vyema mtoto kuwa na nidhamu. Alisema si vyema mtoto kuwa mkatili, mlafi na mchokozi. Mtoto mwenye tabia hizi mbaya huchukiwa na watu wote kijijini.
Siku moja jirani yetu alitutembelea nyumbani kwetu. Jina lake aliitwa Furaha. Furaha alipenda kucheza sana na alikuwa akichukua vitu chumbani bila kuomba mama yake ruhusa kabla ya kubeba.
Ilipofika jioni, Furaha alimwambia mama yake kuwa anahisi njaa na alitaka ale chakula au anywe uji. Mama yake alimwambia asubiri ampikie uji.
Baada ya muda mfupi, Furaha hakusubiri uji uwekewe kwenye kikombe. Alisimama na kujimiminia uji moto mwenyewe. Alipojaribu kunywa, alishindwa. Kwa bahati mbaya, uji moto ulimwagika kwenye nguo zake. Alikimbia mbio huku akilia kwa uchungu mwingi.
Mtoto mwenye tabia mbaya ______ na watu wote.
Answer
Huchukiwa.
Hadithi inasema: "Mtoto mwenye tabia hizi mbaya huchukiwa na watu wote kijijini."
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.