naQonda

CBC Grade 3 Kiswahili Exam Term 2 2025 · Question 36

Kiranja wa darasa la mwandishi ni?

From Kiswahili — Competence Based Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kisha ujibu maswali

Shule yetu inaitwa Osewe. Ina madarasa manane na wanafunzi mia tano hamsini. Walimu wetu ni tisa. Walimu hawa hufanya kazi ya ualimu, yaani kufundisha wanafunzi.
Mwalimu mkuu ni Bwana Hamisi Mwaibale. Yeye ndiye msimamizi mkuu wa shule. Bi Maria ni naibu wa mwalimu mkuu. Yeye humsaidia mwalimu mkuu kusimamia shule haswa katika upande wa nidhamu.
Bi Maria pia ni mwalimu wa darasa letu. Yeye hapendi wanafunzi wanaorandaranda ovyo darasani.
Kiranja wa darasa letu anaitwa Kamau Gitau. Yeye ni mwanafunzi mwenye bidii za mchwa na hufanya vyema darasani. Siku moja, wakati wa mvua hakuweza kubeba vitabu kumpelekea mwalimu.

5. Kiranja wa darasa la mwandishi ni?

Answer

Kamau Gitau

Kifungu kinasema: Kamau Gitau.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 3 Kiswahili questions from this test