naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Revision Exam · Question 1

Mgonjwa anayerejelewa katika habari hii alipatikana na ugonjwa wa

From Test 101 — Revision 6 Kiswahili Karatasi 1 · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu

Kifungu cha Maswali 1–7
Siku moja katika hospitali moja ya kaunti ndogo kuliletwa mgonjwa aliyekuwa
akiumwa na tumbo. Baada ya kuangaliwa kwa makini na kuhojiwa na daktari, alipatikana
na dalili zilizoonyesha ya kuwa alikuwa akiugua ugonjwa wa kipindupindu. Daktari,
wasaidizi wake na wenye mgonjwa walifadhaishwa sana na jambo hili.
Baada ya daktari kuhakikisha maradhi ya yule mgonjwa yalikuwa ni kipindupindu,
alimlaza hospitalini mara moja ili atibiwe hima hima. Yule mgonjwa alikuwa anaendesha
sana huku akitapika kwa njia ya kuhuzunisha.
Punde si punde, yule mgonjwa alitengwa pekee katika chumba kidogo cha kando.
Kwa upendo mwingi na umoja, wauguzi walianza kumhudumia kwa bidii; wakamuuguza
usiku na mchana. Basi kwa neema zake Mwenyezi Mungu na huduma ya wauguzi alianza
kupata nafuu.
Baadaye, daktari alimjulisha mkuu wa kaunti ndogo ya Afya habari hizo huku akitaka
msaada wa kuuangamiza ugonjwa wa kipindupindu ili usisambae na kutisha kaunti nzima.

Mgonjwa anayerejelewa katika habari
hii alipatikana na ugonjwa wa

  1. Awaba
  2. Bkichocho
  3. Cmalale
  4. Dmalaria

Answer

A. waba

The correct option is A.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test