CBC Grade 9 KJSEA Kiswahili Practice Exam · Question 43
Teknolojia imesaidiaje sekta ya kilimo?
From Test 117 — Kiswahili Karatasi ya 1 (902/1 KJSEA) · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha jibu maswali 43 hadi 50 kwa kuchagua jibu sahihi. [Note: Chanzo asilia kilichapisha kichwa cha sehemu hii kama "(Alama 7)", lakini kina maswali 8 halisi yenye majibu 8 yaliyochapishwa mwishoni mwa kijitabu -- imejengwa kama maswali 8 (alama 8); angalia Sehemu C hapo juu kwa hitilafu inayolingana upande wa pili.]
Katika miaka ya hivi karibuni, teknolojia imeendelea kuathiri sekta mbalimbali za maisha. Katika sekta ya kilimo, wakulima sasa wanatumia mbinu za kisasa kama unyunyiziaji wa maji kwa mashine na matumizi ya mbolea za kisasa ili kuongeza uzalishaji wa mazao. Pia, wanatumia simu za mkononi na programu maalum kupata taarifa kuhusu hali ya hewa na masoko ya mazao yao.
Katika sekta ya biashara, wafanyabiashara hutumia mitandao ya kijamii kama WhatsApp, Facebook, na Instagram kutangaza bidhaa zao. Hii imewawezesha kupata wateja wengi kutoka sehemu mbalimbali bila kulazimika kuwa na maduka ya kimwili. Pia, biashara ya mtandaoni imerahisishwa kwa matumizi ya huduma za kifedha kama M-Pesa na benki za kidijitali.
Teknolojia pia imebadilisha mfumo wa ajira. Watu wengi sasa wanaweza kufanya kazi wakiwa nyumbani kupitia kompyuta na intaneti. Mikutano hufanyika mtandaoni kwa kutumia programu kama Zoom na Microsoft Teams, jambo ambalo limepunguza hitaji la safari ndefu kwa ajili ya mikutano.
Licha ya faida hizi, teknolojia ina changamoto zake. Kwa mfano, baadhi ya watu wanapoteza kazi zao kwa sababu mashine zinaweza kufanya kazi ambazo awali zilihitaji binadamu. Pia, kuna tatizo la uhalifu wa mtandaoni kama utapeli na wizi wa pesa kwa njia za kidijitali.
Ni dhahiri kuwa teknolojia ina nafasi kubwa katika maendeleo ya jamii, lakini ni muhimu kutumia kwa tahadhari ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

- AA. Kwa kupunguza matumizi ya mbolea.
- BB. Kwa kutumia mbinu za kisasa kama unyunyiziaji wa maji kwa mashine.
- CC. Kwa kuzuia kilimo cha mazao fulani.
- DD. Kwa kuwazuia wakulima kuuza mazao yao.
Answer
B. B. Kwa kutumia mbinu za kisasa kama unyunyiziaji wa maji kwa mashine.
Jibu sahihi: B. Kwa kutumia mbinu za kisasa kama unyunyiziaji wa maji kwa mashine.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- Kwa mujibu wa kifungu, wafanyabiashara hutumia mitandao ya kijamii kwa sababu gani?Question 44
- Teknolojia imeleta mabadiliko gani katika sekta ya ajira?Question 45
- Ni huduma gani za kifedha zimewezesha biashara za mtandaoni?Question 46
- Gani kati ya hizi sio kifaa cha kielektroniki?Question 47
- Changamoto gani imeletwa na maendeleo ya teknolojia katika sekta ya ajira?Question 48
- Kwa nini ni muhimu kutumia teknolojia kwa tahadhari?Question 49