CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 2
Mojawapo ya magonjwa yanayosababishwa na uchafu ni:
From Kiswahili — First Term Assessment 2025 (Set 7) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Mazungumzo
Soma mazungumzo kati ya mama na mtoto kisha ujibu maswali yafuatayo.
Mtoto: Mama, kwa nini tunapaswa kuweka mazingira yetu safi?
Mama: Tunapaswa kuweka mazingira safi ili kuepuka magonjwa na kufanya eneo letu liwe la kuvutia.
Mtoto: Magonjwa gani yanaweza kusababishwa na uchafu?
Mama: Magonjwa kama vile kipindupindu, malaria na homa yanaweza kusababishwa na uchafu.
Mtoto: Tunawezaje kusaidia kuhifadhi mazingira?
Mama: Tunaweza kusaidia kwa kutupa taka kwenye mapipa, kupanda miti na kuepuka kuchafua maji na hewa.
Mtoto: Asante mama, nitahakikisha ninazingatia hayo!
2. Mojawapo ya magonjwa yanayosababishwa na uchafu ni:
- AShinikizo la damu
- BKifua kikuu
- CKipindupindu
- DUpungufu wa damu
Answer
C. Kipindupindu
Mama anataja kipindupindu, malaria na homa kuwa magonjwa yanayosababishwa na uchafu.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Tunaweza kusaidia kuhifadhi mazingira kwa:Question 3
- Kwa nini ni muhimu kupanda miti?Question 4
- Mtoto alifanya uamuzi gani baada ya mazungumzo na mama yake?Question 5
- SEHEMU B: UFAHAMU 6. Mazingira ni rasilimali muhimu kwa ajili ya:Question 6
- Mazingira safi huleta faida zipi?Question 7
- Shughuli ipi ya binadamu haiharibu mazingira?Question 8