CBC Grade 8 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 10
ZOEZI LA 4: TAMTHILIA (Alama 8) a) Taja sifa mbili za Mwandishi. (Alama 2)
From Kiswahili — KJSEA Assessment 2025, Code 011 (Set 16) · 2 marks · Topic: Kusoma, Tamthilia
Soma mazungumzo yafuatayo ya tamthilia kisha ujibu maswali.
(Waziri na mwandishi wa habari wanazungumza kuhusu ahadi za serikali.)
Mwandishi: Mheshimiwa Waziri, kumekuwa na malalamiko kuwa ahadi nyingi mlizotoa hazijatekelezwa. Hali duni ya barabara, hospitali, na shule inazidi kuwatesa wananchi. Je, mna maelezo gani?
Waziri: (Anatabasamu kwa unyeti) Mpendwa mwandishi, maendeleo ni kama kobe. Huenda polepole, lakini hufika tu. Tunashughulikia suala hili kwa umakini mkubwa. Ni swala la muda tu.
Mwandishi: (Akichukua daftari na kalamu) Lakini kuna tofauti kati ya kobe na ahadi zisizotekelezwa. Kobe hatimaye hufika. Je, ahadi hizi hazitaishia kuwa maneno matupu? Wananchi wanapoteza matumaini.
Waziri: (Akionyesha tabasamu) Ndugu yangu, uvumilivu ndio ufunguo. Tunahitaji ushirikiano wenu ili tufanikishe maono yetu.
ZOEZI LA 4: TAMTHILIA (Alama 8)
a) Taja sifa mbili za Mwandishi. (Alama 2)
Answer
Jasiri: anamkabili Waziri moja kwa moja kuhusu ahadi zisizotekelezwa. Mdadisi: anauliza maswali magumu na kupinga mfano wa kobe.
Mwandishi anamuuliza Waziri maswali magumu bila woga na anapinga jibu lake kwa hoja, akitetea wananchi.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- b) Eleza dhamira kuu ya mazungumzo haya. (Alama 2)Question 11
- c) Taja na ueleze mbinu mbili za lugha zilizotumiwa na Waziri. (Alama 2)Question 12
- d) Eleza matokeo ya ahadi zisizotekelezwa kwa wananchi. (Alama 2)Question 13
- ZOEZI LA 5: USHAIRI (Alama 7) a) Eleza maana ya maneno "Ujana ni bahari." (Alama 2)Question 14
- b) Taja sifa mbili za vijana wa leo kulingana na shairi. (Alama 2)Question 15
- c) Taja dhamira kuu ya shairi hili. (Alama 1)Question 16