CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 14
(b) Mada ya umuhimu wa elimu imeshughulikiwa katika sehemu hii ya tamthilia. Fafanua mada nyingine mbili ambazo zimeshughulikiwa katika sehemu hii ya…
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 4 marks · Topic: Kusoma, Tamthilia
Soma sehemu ifuatayo ya tamthilia kisha ujibu maswali.
SEHEMU 4
Onyesho 1
(Ni jioni, ndani ya nyumba ya Bi. Zawadi. Mezani kuna vitabu na kalamu. Bi. Zawadi anamsaidia mwanawe, Kaka, kufanya kazi za nyumbani. Kaka anaonekana kuchoka na kukosa ari.)
Bi. Zawadi: (Kwa sauti ya upole) Kaka mwanangu, umalize kazi zako za shule. Kesho una mtihani muhimu.
Kaka: (Akiguna) Mama, nimechoka sana. Na somo hili la Hisabati ni gumu sana. Sielewi kabisa.
Bi. Zawadi: (Akimwangalia kwa upendo) Usikate tamaa mwanangu. Kila kitu kigumu mwanzoni huwa rahisi baadaye ukijitahidi. Kumbuka methali isemayo, Hamna marefu yasiyokuwa na ncha.
Kaka: Lakini mama, siwezi. Walimu hawafundishi vizuri. Na wanafunzi wengine wananielewa haraka.
Bi. Zawadi: Kaka, usilinganishe na wengine. Kila mtu ana kasi yake ya kujifunza. Muhimu ni wewe kujitahidi na kuuliza maswali pale unapokwama. Unaweza kumuuliza Mwalimu Juma, yeye ni mtaalamu wa Hisabati.
Kaka: (Akifikiria) Kweli?
Bi. Zawadi: Ndiyo. Na mimi niko hapa kukusaidia. Tutafanya kazi hii pamoja. Nikuoneshe jinsi ya kufanya hizi namba.
(Bi. Zawadi anaanza kumwelekeza Kaka. Kaka anaanza kuonesha tabasamu la aibu, akijaribu kuelewa. Taratibu, anaelewa.)
Kaka: Asante sana mama! Sasa nimeelewa! Kumbe siyo ngumu hivi!
Bi. Zawadi: (Akimkumbatia) Hongera mwanangu. Hiyo ndiyo roho. Kujitahidi na kusaidiana. Elimu ni muhimu sana, itakufungulia milango mingi maishani.
(Taa zinazimika polepole, ikionesha kuwa wataendelea kujifunza.)
(b) Mada ya umuhimu wa elimu imeshughulikiwa katika sehemu hii ya tamthilia. Fafanua mada nyingine mbili ambazo zimeshughulikiwa katika sehemu hii ya tamthilia. (alama 4)
Answer
Malezi bora: Bi. Zawadi anamhimiza Kaka kwa upole, anaketi naye na kumwelekeza Hisabati hadi anaelewa. Uvumilivu na kutokata tamaa: Kaka anataka kukata tamaa kwa sababu Hisabati ni ngumu, lakini mama yake anamtia moyo na mwishowe anaelewa.
Mada nyingine ni kama malezi na wajibu wa mzazi, uvumilivu na kutokata tamaa, ushirikiano au kusaidiana, na kutojilinganisha na wengine (kila mtu ana kasi yake ya kujifunza).
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- (c) Eleza umuhimu wa maelezo yaliyoandikwa kwa herufi za mlazo (yaliyo kwenye mabano) katika sehemu hii ya tamthilia.…Question 15
- (d) Neno ‘kuguna’ ni mfano wa mbinu ya onomatopeia. Eleza mbinu nyingine mbili za lugha zilizotumiwa katika sehemu hii…Question 16
- ZOEZI V: USHAIRI (Alama 5) (a) Eleza ujumbe wa shairi hili. (alama 2)Question 17
- (b) Ni wahusika gani wanashauriwa katika shairi hili? (alama 1)Question 18
- (c) Bainisha mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika ubeti wa kwanza. (alama 2)Question 19
- SEHEMU A (Alama 15) ZOEZI I: INSHA Maagizo i. Inapendekezwa uchukue muda wa dakika 40 katika zoezi hili. ii. Andika…Question 1