CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 4
c) Tambulisha aina mbili za mandhari zinazojitokeza katika simulizi hii. (Al 2)
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 2 marks · Topic: Fasihi, Mandhari
SEHEMU B: FASIHI SIMULIZI (Alama 10)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Katika milima ya Upweke, kuliishi jamii ya Wanyenyekevu iliyostawi kwa amani. Kijiji chao cha Tulivu kilikuwa pepo ya duniani; mito ilicheka kwa furaha na upepo ulivuma kwa upole ukibeba harufu ya maua ya mchanasoke. Hata hivyo, mambo yaligeuka ghafla. Jua likaanza kutoa macho ya hasira, ardhi ikapasuka kwa kiu na mimea ikainamisha vichwa kwa unyonge. Njaa ikawa mgeni asiyealikwa aliyebisha hodi katika kila nyumba.
Wazee wa kijiji walijikusanya chini ya mti wa Mvule-Busara kutafuta suluhu. Hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba hata ndege walisita kuimba. Katika ukimwi huo wa huzuni, alisimama shujaa mmoja kwa jina Sauti-ya-Radi. Alikuwa mwanamume mwenye kifua kipana kama uwanja wa michezo na macho yaliyoonekana kubeba mwanga wa mwezi. Inasemekana alirithi kipaji cha kuamuru mawingu kutoka kwa babu yake, mzee Mvua-Nyingi.
Siku ya pili, Sauti-ya-Radi alipanda kilele cha mlima Mrefu-Sana. Alipofika kileleni, alinyosha mikono yake kuelekea mbinguni, akafunga macho, na kuanza kuimba wimbo wa maombi uliotetemesha miamba. Machozi yake yalidondoka kama lulu nyekundu:
Enyi wajenzi wa anga, Mlioshika funguo za milango, Kwetu kiu imekuwa donda, Ardhi yalia kwa uchungu. Fungueni vifungo vya mvua x2. Watoto wamepoteza tabasamu, Mifugo yetu inakata roho, Kwa wimbo huu na ombi langu, Shusheni baraka za maji, Fungueni vifungo vya mvua x2
Ghafla, anga lililokuwa kavu lilianza kutanda mawingu mazito ya kijivu. Ngurumo za radi zilijibu wimbo wake kwa kishindo. Mvua ilianza kunyesha kwa wingi, siyo kama hasira bali kama baraka. Wanyenyekevu walitoka nje na kucheza, huku Sauti-ya-Radi akibaki kileleni, akiwa ameloa chapachapa lakini moyo wake ukiwa na utulivu.
Sauti-ya-Radi hakuwa mtu wa kujitapa; aliamini kuwa mcheza kwao hutuzwa. Uwezo wake uliendelea kuwa kinga ya kijiji hicho dhidi ya majanga ya asili. Alipoaga dunia baada ya miaka mingi, alimwachia binti yake, Chemchemi, uwezo huo kupitia kishaufu cha dhahabu kilichokuwa na nguvu za ajabu. Hadi leo, hadithi za ushujaa wake zinatambaa kwenye ndimi za kila kizazi katika kijiji cha Tulivu.
c) Tambulisha aina mbili za mandhari zinazojitokeza katika simulizi hii. (Al 2)
Answer
Mandhari ya mahali: Milima ya Upweke, Kijiji cha Tulivu na kilele cha mlima Mrefu-Sana. Mandhari ya hali: simanzi ya ukame inayogeuka kuwa furaha.
Mandhari ni mahali, wakati au hali.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- d) Eleza umuhimu wa mhusika Sauti-ya-Radi katika jamii yake. (Al 2)Question 5
- e) Iwapo ungeombwa kuwasilisha hadithi hii mbele ya darasa, ungetumia mbinu gani mbili za utendaji? (Al 2)Question 6
- a) Kazi ya fasihi huwa na madhumuni maalum. Fafanua madhumuni ya sehemu hii ya novela. (al 2)Question 7
- b) Ufukara ni mandhari ya hali inayojitokeza katika sehemu hii ya novela. Eleza aina nyingine mbili za mandhari…Question 8
- c) Baraka ni mhusika mkarimu. Bainisha sifa nyingine mbili za Baraka. (al 2)Question 9
- d) Ploti ni mtiririko wa matukio katika kazi ya fasihi. Eleza mfuatano wa matukio muhimu katika aya ya nne na ya tano.…Question 10