CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 11
e) Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika sehemu hii ya novela. (al 2)
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 2 marks · Topic: Fasihi, Mbinu za Lugha
NOVELA (Alama 10)
Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali.
Kijiji cha Mizizi kimegonga vichwa vya habari nchini kufuatia hatua kubwa ya kimaendeleo iliyofikiwa katika sekta ya kilimo biashara. Hii si mara ya kwanza kwa kijiji hiki kupata sifa tele. Kwa miaka mitano mfululizo, wakulima wa hapa wamekuwa wakiongoza kwa uzalishaji wa zao la kahawa. Mafanikio haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na Baraka, kijana mbunifu aliyetunukiwa nishani ya mwanasayansi chipukizi wa mwaka.
Baraka ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia ya Bwana na Bi. Subira. Katika familia hiyo, ufukara ulikuwa umepiga kambi na kutandika jamvi, lakini Bwana Subira na mkewe walikula mbuni ili kuhakikisha wana wao wanapata elimu. Malezi waliyowapa yalikuwa ya kupigiwa mfano; yalijengwa juu ya misingi ya unyenyekevu. Baraka na dada yake walikuwa na bidii ya mchwa iliyowawezesha kupenya katika kuta nene za umaskini. Dada yake alibobea katika sheria, naye Baraka akang'aa katika masomo ya sayansi na teknolojia.
Shuleni, Baraka alitambulika mapema na mwalimu wa sayansi kwa kuwa alikuwa na uwezo wa kuunda mashine ndogondogo kwa kutumia vifaa vilivyotupwa. Akiwa katika gredi ya saba, mwalimu mkuu alimteua kuwa kiongozi wa klabu ya mazingira. Jukumu hilo alilitekeleza kwa jasho na damu. Katika mashindano ya kitaifa ya uvumbuzi, Baraka aliongoza shule yake kwa kuunda mtambo wa kusafisha maji na kuibuka mshindi wa kwanza.
Baraka hakuingiliwa na upepo wa kiburi masomoni. Baada ya kuhitimu elimu ya upili kwa alama za juu, alifaulu na kujiunga na chuo kikuu cha kiteknolojia nchini. Alifadhiliwa kimasomo na Kampuni ya Nuru iliyokuwa ikisaidia wanafunzi wenye akili bongo. Kampuni hiyo ilikuwa na mradi uitwao 'Elimu ni Mwanga.' Ufadhili huo uliiondolea familia yake mzigo wa madeni na kuwapa tabasamu la kudumu. Katika kongamano la kimataifa la wabunifu, Baraka alitambulika na wataalamu wa kilimo. Aliteuliwa kujiunga na jopo la watafiti wa mbegu; Kizazi-Kipya. Kumbuka, Baraka alijiunga na jopo hilo akiwa bado ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu. Wenzake walimbandika jina 'Taa' kutokana na uwezo wake wa kutoa suluhu kwa matatizo magumu ya kijamii.
Baraka amepokea tuzo mbalimbali ikiwemo ile ya 'Mbunifu Bora wa Afrika.' Hali hii imemfungulia milango ya heri na kumpa nafasi ya kusafiri ulimwenguni kote. Mapato yake yamemwezesha kuwajengea wazazi wake nyumba ya kisasa na kuanzisha mradi wa maji kijijini kwao. Aidha, amekuwa akichangia mfuko wa 'Elimu ni Mwanga' ili kusaidia watoto wengine maskini. Kijiji cha Mizizi kinajivunia kuwa na lulu kama hii. Wengi husema Baraka alizaliwa na nyota ya kijani. Ukimwuliza mamake, atakuambia kuwa Baraka alivuna alichopanda. Amekuwa balozi wa kusisitiza kuwa elimu ni ufunguo wa maisha.
e) Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika sehemu hii ya novela. (al 2)
Answer
Tashbihi: "bidii ya mchwa". Nahau: "walikula mbuni".
Tafuta ulinganisho na semi.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- a) Bainisha aina mbili za mandhari katika sehemu hii ya tamthilia. (al 2)Question 12
- b) Eleza mambo mawili yaliyoangaziwa katika sehemu hii ya tamthilia. (al 2)Question 13
- c) Fafanua sifa za Shibe kama zinavyojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia. (al 2)Question 14
- d) Eleza umuhimu wa maneno yaliyotiwa kwenye mabano katika sehemu hii ya tamthilia. (al 2)Question 15
- e) Mbinu ya nahau imetumiwa katika sehemu hii ya tamthilia. Tambulisha mbinu nyingine mbili za lugha. (al 2)Question 16
- a) Eleza dhamira ya shairi hili. (al 1)Question 17