CBC Grade 7 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 15
Ni huduma gani moja ya muhimu inayotolewa na serikali?
From Kiswahili — KJSEA Assessment 2025, Code 011 (Set 14) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 13 hadi 17:
Serikali ni mfumo wa utawala unaosimamia nchi au eneo fulani. Kuna aina mbalimbali za serikali, lakini jukumu kuu la kila serikali ni kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi wake. Huduma hizi ni pamoja na afya, elimu, usalama, na ujenzi wa miundombinu kama barabara na madaraja. Serikali hufanya kazi kupitia wizara na idara mbalimbali zinazosimamia sekta tofauti.
Wananchi wana jukumu la kushirikiana na serikali yao. Hii inajumuisha kulipa kodi, kutii sheria, na kushiriki katika uchaguzi. Kwa kufanya hivyo, wananchi huwezesha serikali kutoa huduma bora na kutekeleza miradi ya maendeleo. "Mkono mmoja haupigi kofi", na hivyo ushirikiano kati ya serikali na wananchi ni muhimu.
15. Ni huduma gani moja ya muhimu inayotolewa na serikali?
- AMichezo ya Soka.
- BUsafiri wa ndege.
- CElimu.
- DUtalii.
Answer
C. Elimu.
Huduma zilizotajwa ni afya, elimu, usalama na ujenzi wa miundombinu; elimu ni mojawapo.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Kwa nini wananchi wanashauriwa kulipa kodi?Question 16
- Methali "Mkono mmoja haupigi kofi" inamaanisha nini katika muktadha wa kifungu?Question 17
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 18.Question 18
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 19.Question 19
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 20.Question 20
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi ya 21.Question 21