naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 4

Uharibifu wa misitu na makazi ya wanyama unasababisha nini?

From Kiswahili — KJSEA Assessment 2025, Code 010 (Set 13) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 1 hadi 6:

Wanyama pori ni sehemu muhimu ya mfumo wa ikolojia na utalii. Baadhi yao ni wakubwa na wenye nguvu kama simba, chui, na tembo. Wengine ni wadogo na wa haraka kama swala na sungura. Kila mnyama ana jukumu lake katika mazingira. Simba husaidia kudhibiti idadi ya wanyama wengine, na hivyo kuzuia mazingira kuharibika. Nyuki na vipepeo, ingawa ni wadogo, huchangia pakubwa katika uchavushaji wa mimea.

Wanyama hawa wanakabiliwa na changamoto nyingi. Ujangili, au uwindaji haramu, ni tishio kubwa. Wengine wanatafutwa kwa pembe zao au meno yao, na hivyo kupelekea idadi yao kupungua. Uharibifu wa misitu na makazi yao pia unawaathiri vibaya. Serikali na mashirika mbalimbali yameanzisha hifadhi za wanyama na mbuga za kitaifa ili kuwalinda. Elimu kuhusu umuhimu wa wanyama pori inahitajika ili kila mtu aelewe jukumu lake katika uhifadhi.

4. Uharibifu wa misitu na makazi ya wanyama unasababisha nini?

  1. AWanyama wanaongezeka.
  2. BWanyama wanahamia miji.
  3. CWanyama wanaathirika vibaya.
  4. DWanyama wanapata chakula kingi.

Answer

C. Wanyama wanaathirika vibaya.

Kifungu kinasema uharibifu wa misitu na makazi yao unawaathiri vibaya wanyama.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test