naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 1 2026 · Question 10

c) Eleza hulka ya baba yake Chale.(Alama 3)

From Kiswahili — Term 1 Assessment 2026 (Set 1) · 3 marks · Topic: Kusoma, Novela

SEHEMU C: NOVELA (Alama 11)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Walikimbia hadi walipopata upenyo wa kuingia. Waliendelea kushangilia bila kuchoka. Chale alisimama kwenye ukingo wa bwawa akitazama safari yake ya mchana mzima. Mara, wenzake wote walikuwa wameondoka.
Alipotoka bwawani, aliangalia huku na kule asione mtu. Aliona watoto wadogo wakicheza pembeni, wakiwa na furaha. Chale alibaki kimya, akihisi uchovu na huzuni moyoni.
“Tumekwisha!” alisema kwa sauti ya chini huku akivaa gwanda moja lililomsitiri vizuri. Aligeuka kutaka kuelekea nyumbani na ghafla akajikuta akitazamana uso kwa uso na baba yake. Macho ya baba yalionyesha hasira na huzuni.
Chale alitabasamu kwa aibu, akijipa moyo kwamba kama kungekuwa na jambo la kueleza, angefanya hivyo nyumbani.

c) Eleza hulka ya baba yake Chale.(Alama 3)

Answer

Ni mkali (macho yalionyesha hasira), anayejali mwanawe (alikuja kumtafuta), na mwenye huzuni kwa tabia ya mwanawe.

Hulka ni tabia; itoe kwa ushahidi.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test