CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2025 · Question 32
e. Andika kichwa cha shairi hili.
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2025 (Set 13) · 1 mark · Topic: Ushairi, Shairi
12. Soma shairi hili na ujibu maswali.
Yamepita ya zamani, 'mebadilika
Ondoka twende shuleni, dada nanyi kina kaka
Msibaki majumbani, mwisho mtahangaika
Elimu ndiyo maisha, vijana wote someni
Tuanzie vijijini, kuliko sahaulika
Tujiondoe gizani, maisha 'mebadilika
Twende shule tusomeni, kuchora na kuandika
Elimu ndiyo maisha, vijana wote someni
Sikubali asilani, kuacha shule kuolewa
Au kwenda baani, kunywa pombe na vibaka
Ukimwi upo njiani, ukicheza utakushika
Elimu ndiyo maisha, vijana wote someni.
e. Andika kichwa cha shairi hili.
Answer
Elimu Ndiyo Maisha
Kibwagizo kinaeleza ujumbe mkuu: elimu ni maisha.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- f. Katika ubeti wa kwanza, mshororo wa mwisho una mizani mingapi?Question 33
- Pengo 1: andika neno kutoka kisandukuni.Question 34
- Pengo 2: andika neno kutoka kisandukuni.Question 35
- Pengo 3: andika neno kutoka kisandukuni.Question 36
- Pengo 4: andika neno kutoka kisandukuni.Question 37
- Pengo 5: andika neno kutoka kisandukuni.Question 38