CBC Grade 4 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 1
Soma kifungu hiki kwa sauti.
From Kiswahili — KPSEA School Based Assessment 2025 (Set 11) (Kusoma kwa Sauti) · 20 marks · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Sauti
Shangazi alituandalia chakula kilichonukia kama ruhani. Alitukaribisha mezani. Kila mmoja aliketi umbali wa mita moja na nusu kutoka kwa mwenzake. Tulizingatia maagizo ya Wizara ya Afya. Kaka aliombea chakula kisha tukanawa mikono. Kila mmoja alijipakulia chakula kiasi cha kumtosha.
Shangazi alitupongeza kwa kuzingatia adabu mezani. Alitupongeza tulivyokula kwa heshima. Aidha, alisema tumelelewa vizuri. Hakuna aliyebakisha chakula kwenye sahani. Shangazi alitushukuru nasi tukamuahidi kumtembelea tena.
Soma kifungu hiki kwa sauti.
Answer
Shangazi Naomi hututembelea kwetu kila likizo. Likizo iliyopita, nasi tuliruhusiwa kwenda kumtembelea. Tulimpelekea sukari, unga na matunda. Shangazi alifurahi sana. Mimi na kakangu pia tulifurahi kumwona. Shangazi alituandalia chakula kilichonukia kama ruhani. Alitukaribisha mezani. Kila mmoja aliketi umbali wa mita moja na nusu kutoka kwa mwenzake. Tulizingatia maagizo ya Wizara ya Afya. Kaka aliombea chakula kisha tukanawa mikono. Kila mmoja alijipakulia chakula kiasi cha kumtosha. Shangazi alitupongeza kwa kuzingatia adabu mezani. Alitupongeza tulivyokula kwa heshima. Aidha, alisema…
Soma kila neno wazi na kwa usahihi, kama vile tuliruhusiwa, kilichonukia, alijipakulia na tumelelewa. Simama kidogo kwenye koma na vituo, na usome kwa kasi inayofaa kutoka mwanzo hadi mwisho.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.