CBC Grade 3 Kiswahili Mock Exam 2025 · Question 8
Alitaka wananchi wafanye nini?
From Kiswahili — Competence Based Assessment First Trial 2025 (Set 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
SEHEMU YA 3: UFAHAMU
Soma ufahamu huu kisha ujibu maswali
MFALME MJINGA
Siku Moja mfalme mjinga aliitisha mkutano. Wananchi wake walikusanyika kwa wakati uliopangwa. Katika mkutano huo aliwataka wananchi wake kufanya mambo yao kwa ushirikiano. Aliwataka maskini wote wasaidie wasiojiweza. Vilevile, aliamuru kuvunjwa kwa nyumba za kisasa. Mfalme mjinga aliwakumbusha wananchi wake kupunguza vyumba na madarasa. Halafu, mfalme mjinga aliwahimiza wananchi wake kung’oa miti mbalimbali katika mazingira yao. Wananchi wote walikasirika, hivyo waliona ishara ya kumuuma mkono.
2. Alitaka wananchi wafanye nini?
Answer
wafanye mambo yao kwa ushirikiano
Aliwataka wananchi kufanya mambo yao kwa ushirikiano.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.